BERLIN Fischer akutana na Geldorf mjini Berlin
13 Juni 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Joschka Fischer alikutana na muimbaji mashuhuri wa miondoko ya pop, Sir Bob Geldof, mjini Berlin hapa Ujerumani. Muimbaji huyo amekuwa msitari wa mbele kuongoza kampeni ya kuuangamiza umaskini na magonjwa barani Afrika.
Katika mazungumzo yao walijadili vipi Ujerumani inavyoweza kusaidia juhudi za maendeleo barani Afrika. Mkutano huo wao ulifanyika baada ya mawaziri wa fedha kutoka mataifa yaliyoendelea zaidi kiviwanda duniani, G8, kukubaliana kuyafuta madeni ya kiasi cha euro bilioni 30 kwa mataifa maskini zaidi barani Afrika.
Waafrika na mashirika ya misaada duniani yameyapongeza mataifa ya G8 kwa hatua hiyo lakini yakasisitiza kuna kazi kubwa zaidi inayotakiwa kufanywa.