BERLIN: Dhamiri izushayo mvutano ya kuuza kiwanda cha kijerumani cha
8 Desemba 2003Matangazo
kutengenezea PLUTONIUM kwa China, imezusha majadiliano makali mjini Berlin. Kansela Gerhard Schroeder alisema jana kuwa hatarudi nyuma kuhusika na biashara hii, na hakujali lawama za chama cha Kijani kikishiriki serikali yake ya muungano. Kinu hiki cha kinyuklia kikimilikiwa na kampuni SIEMENS, kipo karibu na Frankfurt. Biashara hii na serikali ya China inakisiwa kugharimu EURO Millioni 50. Chama cha Kijani kimeahidi kutumia njia zote za kisheria na kisiasa ili kuzuia uuzaji.