Berlin. Chama kipya chaahidi kuwalinda wanyonge.
27 Agosti 2005Wiki tatu kabla ya uchaguzi mkuu wa Ujerumani , chama kipya cha mrengo wa kushoto kimesema katika mkutano wake mkuu leo kuwa ilani yake ya uchaguzi inayolenga katika kulinda maslahi ya kijamii i nawezekana kifedha.
Rais wa chama hicho Lothar Bisky amesema kuwa dhana hiyo si kuwa inaelea tu mawinguni.
Amesema kuwa inawezekana kuwa na fedha za mpango huo, ambao unataja kuwa na mshahara wa kiwango cha chini, kiwango cha akiba ya uzeeni cha kiwango cha chini pamoja na msamaha wa kodi kwa muda kwa wale wanaopata kiwango cha chini cha mishahara, iwapo serikali itaweza kuwafanya wale wenye kipato cha juu na wale wenye mishahara mikubwa kuchangia katika unafuu wa maisha kwa jamii.
Chama hicho kinaundwa na Wakomunist wa zamani katika iliyokuwa Ujerumani ya mashariki na wanachama wa zamani chama tawala cha Social Democrats ambao walijiuzulu kutokana na mpango wa kansela Schröder wa kwenda mapumziko katika kisiwa cha kifahari katika bahari ya Mediterranean cha Majorca.