BERLIN: Bush ziarani barani Ulaya.
23 Februari 2005Rais Gorge Bush wa Marekani amefanya mazungumzo na Kasela wa Ujerumani Gerhard Schroeder mjini Mainz katika ziara yake barani ulaya. Katika mkutano huo Bush amezungumzia zaidi juu ya kuimarisha uhusiano na masuala ya kimataifa ikiwa ni pamoja na suala la mpango wa silaha za nuklear wa Iran.Bush pia alizungumzia kuhusu wito uliotolewa na Ujerumani wa kutaka kufanywa mabadiliko katika NATO.
Kansela Gerhard Schroder alisema amefurahishwa na hatua ya marekani ya kuunga mkono juhudi za umoja wa Ulaya za kuishawishi Iran kuachana na mpango wa kutengeneza silaha za kinuclear.Kuhusu suala la Syria Busha alisema anasubiri kuona ya iwapo itakubali kufuata agizo la kutaka kuwaondoa wanajeshi wake wote kutoka Lebanon kabla ya kuutaka Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo serikali ya Damascus,jambo ambalo Schroeder aliliunga mkono.
Maelfu ya watu wameandamana mjini Mainz dhidi ya ziara ya Bush Ujerumani huku wakibeba mabango yalioandikwa kiongozi wa vita nenda nyumbani .Bush amepangiwa kufika Bratislava nchini Slavak baadae hii leo na hapo kesho atakutana na rais Vladmir Putin wa Russia.