BERLIN: Binadamu waendelea kuongezeka duniani
9 Agosti 2006Matangazo
Idadi ya watu ulimwenguni inaendelea kuongezeka kwa haraka.Mwaka huu kuna watu milioni 80 zaidi kulinganishwa na hesabu za mwaka uliopita.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya inayotolewa kila mwaka na wakfu wa Kijerumani unaoshughulika na idadi ya watu duniani.Ripoti hiyo inasema duniani sasa idadi ya watu ni bilioni 6.6 na idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka hadi bilioni 7 katika kipindi cha miaka sita ijayo.Muongezeko mkubwa unatokea nchi zilizo masikini,wakati madola tajiri yalioendelea kiviwanda yanashuhudia idadi ya raia wake ikipunguka.