BERLIN Bibi Merkel aahidi kusema ukweli
31 Mei 2005Matangazo
Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha CDU bibi Angela Merkel aliyeteuliwa na chama chake kugombea wadhifa wa Ukansela amevitaka vyama vya upinzani viendeshe kampeni katika msingi ya kusema ukweli.
Bibi Merkel amesema kwamba vyama hivyo vinapaswa kutoa ahadi zinazoweza kutekelezwa, aidha ameeleza kwamba, ni lazima kutamka wazi, juu ya mambo yanayoweza kufanyiwa mageuzi.
Mwanasiasa huyo atakaekuwa mwanamke wa kwanza kugombea wadhifa wa ukansela hapa nchini Ujeumani pia ametilia maanani kwamba Ujerumani imo katika kinyangànyiro kigumu cha kimataifa.
Hatahivyo bibi Merkel ameahidi kuondosha urasimu unaokinza ustawi wa uchumi.
.