BERLIN. Bibi Angela Merkel ajikakamua katika kampeini
29 Agosti 2005Vugu vugu za kampeni zinazidi kushika kasi hapa nchini Ujerumani huku yakiwa yamesalia majuma matatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa bunge.
Bibi Angela Merkel mgombea wa kiti cha Ukansela wa Ujerumani katika kampeni yake ameahidi kuikwamua nchi yake kutoka kwenye mzozo wa kiuchumi.
Kenye hotuba yake mjini Dortmund, bibi Merkel wa chama cha upinzani cha CDU alimlaumu kansela Gerhard Schröder na serikali yake ya muungano kwa kushindwa kuiweka Ujerumani katika maendeleo ya kisasa hatua mabayo imewanyima nafasi za kazi takriban watu milioni tano.
Vile vile wajumbe wa chama cha CDU wamemu idhinisha meneja wao wa shughuli za kampeini bwana Volker Kauder kama katibu mkuu wa chama hicho cha CDU.
Kansela Gerhard Schröder anaulaumu mikakati ya marekebisho ya sheria za wafanya kazi na kuongeza kodi ya mapato kama hatua itakayoleta hali ngumu ya maisha na kwa uchumi wa Ujerumani
Kura ya maoni inaonyesha bibi Angela Merkel anaendelea kupata umaarufu zaidi kwa asilimia 42 dhidi ya Kansela Schröder ambae ana asilimia 29.