BERLIN. Baraza la mawaziri wakuu kuipigia kura katiba ya Umoja wa Ulaya.
27 Mei 2005Matangazo
Baraza la mawaziri wakuu wa majimbo ya Ujerumani – Bundesrat linakutana mjini Berlin kuipigia kura katiba ya Umoja wa Ulaya.
Wadadisi wanaamini kuwa baraza hilo litaidhinisha katiba hiyo.
Katiba hiyo ya Umoja wa Ulaya imeshapigiwa kura na bunge la shirikisho – Bundestag wiki mbili zilizopita.
Mwenyekiti wa kamisheni ya mageuzi ya taasisi za Umoja wa Ulaya muasisi wa katiba hiyo rais wa zamani wa Ufaransa Valery Giscard d’Estain ni miongoni mwa wanasiasa wanaotazamiwa kuhutubia mbele ya Bundesrat hii leo.
Ujerumani ni nchi ya tisa ya Umoja wa Ulaya kuidhinisha katiba hiyo ili iweze kufanya kazi.
Katiba hiyo inabidi iidhinishwe na nchi zote 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya.