BERLIN: Angela Merkel aanza kampeni za ukansela
11 Agosti 2005Matangazo
Kiongozi wa chama cha Christian Democratic Union, CDU, Bi Angela Merkel, ameanza kampeni ya kugombea wadhifa wa ukansela hapa Ujerumani. Merkel ameanza kwa mkutano wa hadhara katika mji wa viwanda wa Essen, magharibi mwa Ujerumani.
Ijapo Merkel anaongoza katika kura ya maoni, kuungwa mkono kwake kumepungua baada ya kushindwa kutofautisha maswala ya kiuchumi katika mahojiano yaliyoonyeshwa kwenye runinga. Anajaribu sasa kuziongozea nguvu juhudi zake za kampeni kwa kuwa na mikutano kadhaa ya hadhara katika siku chache zijazo.