Benki ya AfDB kuchagua rais mpya
27 Mei 2025Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB inamchaguwa rais wake mpya Alkhamisi, katika mkutano unaofanyika nchini Ivory Coast.
Mkutano huo unafanyika wakati benki hiyo ambayo ni mkopeshaji mkubwa wa mataifa ya bara hilo ikikabiliwa na changamoto ambazo hazikutegemewa kutokana na hatua ya Marekani kuiondolea ufadhili.
Washington inataka kukata ufadhili wa dola milioni 555 kwa benki hiyo pamoja na mfuko wake wa maendeleo kwa Afrika ambao unatoa mkopo nafuu kwa mataifa masikini ya bara hilo.
Mkutano wa viongozi wakuuwa nchi na taasisi za fedha unaofanyika mjini Abidjan ni moja ya mikutano mikubwa ya kifedha ndani ya bara hilo.
Mkutano huo utamchagua rais mpya wa AfDB atakayechukuwa nafasi inayoshikiliwa sasa na Akinwumi Adesina atakayeondoka mwezi Septemba baada ya kukamilisha muda wake wa miaka mitano.
Wagombea watano wamejitokeza kutoka Afrika Kusini, Senegal, Zambia, Chad na Mauritania.