Belfast: Kwa mujibu wa matokeo ya mwanzo, vyama vya siasa kali...
28 Novemba 2003Matangazo
katika upande wa Waprotestanti na ule wa Wakatholiki vimepata nguvu katika uchaguzi wa mkoa wa Ireland ya Kaskazini. Walipoulizwa wapigaji kura baada ya kutumbukiza kura zao, yaonesha Chama cha Sinn-Fein ambacho kiko karibu na Jumuiya ya kikatholi inayoendesha shughuli zake chini kwa chini, IRA, kitapata karibu asilimia 20 ya kura. Chama cha siasa za wastani cha Social Democratic na Labour, ambacho hapo kabla kilikuwa chama chenye nguvu miongoni mwa vile vinavopendelea Ireland ya Kaskazini iwe huru, yaonesha kitapata asilimia 16 ya kura. Kwa mujibu wa maoni ya watu walioulizwa baada ya uchaguzi, chama cha siasa kali katika kambi ya Waprotestanti, kitapata asilimia 25 ya kura. Kwa hivyo vyama ambavyo viliyakataa mapatano ya amani ya mwaka 1998 vina nguvu sawa na chama cha Waprotestanti wenye siasa za wastani, Chama cha Unionist cha waziri kiongozi David Tremble.