BELFAST-IRA yatakiwa kusimamisha harakati za kijeshi dhidi ya Uingereza.
7 Aprili 2005Matangazo
Rais wa chama cha siasa cha Sin Fein katika Jamhuri ya Ireland,Gerry Adams,amekitaka kikosi chake cha jeshi la IRA,kusimamisha harakati za kijeshi dhidi ya utawala wa Kiingeraza huko Ireland ya Kaskazini.
Katika barua ya wazi iliyosomwa katika televisheni,Bwana Adams amewataka wanajeshi wa IRA kujijumuisha katika mchakato wa kisiasa na kuachana na vitendo vya hujuma.
Kkundi cha Sin Fein hivi karibuni kimekuwa katika shinikizo kubwa la kisiasa kutokana na kuwepo madai ya jeshi la IRA kujihusisha na vitendo vya kihalifu.