Beirut: Wanaoshukiwa kutaka kuripua treni hapa Ujerumani washtakiwa Libanon.
3 Septemba 2006Matangazo
Kutokana na jaribio lililoshindwa la kuripua reli za kimkoa hapa Ujerumani, mkuu wa kuendesha mashtaka huko Libanon amewashtaki Walibanon watano na Msyria mmoja. Wanne kati ya washukiwa hao wamewekwa vizuizini huko Libanon na wawili hapa Ujerumani. Polisi hapa Ujerumani wanajaribu kutaka hao waliokamatwa Libanon waletwe Ujerumani. Idara ya upepelezi ya hapa Ujerumani, kwa mara ya kwanza , imeyataja madhumu ya washukiwa hao. Mkuu wa idara hiyo, Jörg Ziercke, amesema kuchapishwa picha za kumkashifu Mtume Mohammad ndio kilikua kichocheo cha nia ya watu hao. Sababu nyingine ni kufa kwa kiongozi wa magaidi, Abu Mussab al-Zarkawi, huko Iraq hapo Juni mwaka huu.