BEIJING:Schroeder ziarani China
1 Desemba 2003Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amewasili nchini China leo hii kwa ziara rasmi ya siku nne yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya washirika wawili wa kibiashara na kutumia vizuri uwezo mkubwa ulioko China wa kuagizia bidhaa kutoka nje. Ziara hiyo ya Schroeder ni ya tano nchini China ina inakuja wakati biashara kati ya nchi hizi mbili ikizidi kunawirika juu ya kwamba masuala ya kidiplomasia kama vile Iraq na Korea Kaskazini yanatarajiwa kuwemo katika agenda yake. Schroeder atakutana na Rais Hu Jintao wa China na Waziri Mkuu Wen Jiabao baadae leo kabla ya kuelekea Guangdong na Chengdu hapo kesho. Waziri wa Sheria Brigite Zypries na Waziri wa Uchukuzi Manfred Stolpe wanaandamana na Schroeder katika ziara hiyo ambayo pia inawajumuisha wakuu 38 wa makampuni makubwa kabisa ya Kijerumani kama vile Siemens,Volkswagen Bayer na Commerzbank.