BEIJING:Schroeder leo kukamilisha ziara China
3 Desemba 2003Matangazo
Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani leo anatazamiwa kuutembelea mji wa magharibi wa China Chengdu. Hicho kitakuwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake ya siku tatu nchini China na ambapo Ujerumani inapanga kuanzisha ofisi ndogo mpya ya ubalozi katika mji huo.Lengo kuu la ziara ya Schroeder ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi mbili hizi.Hapo jana Schroeder na takriban viongozi 40 wa kibiashara wanaoandamana naye katika safari hiyo walihudhuria onyesho la magari mjini Guangzhou.Majimbo hayo ya China ni mojawapo ya maeneo yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani. Biashara ya Ujerumani na maeneo hayo kwa hivi sasa inafikia zaidi ya euro bilioni tano kwa mwaka.