Beijing. Watu laki sita wahamishwa kwa hofu ya kimbunga.
19 Julai 2005Matangazo
Zaidi ya watu 600,000 kutoka katika maeneo ya pwani nchini China wameondolewa wakati kimbunga Haitang kinakaribia huku kukiwa na mvua kubwa pamoja na upepo.
Hapo kabla kimbunga hicho kiliikumba taiwan , na kusababisha mafuriko na kulazimisha kufungwa kwa shule, ofisi na masoko katika kisiwa hicho.
Kiasi watu wanne wanaripotiwa kuwa wameuwawa na dhoruba hiyo.
Watabiri wa hali ya hewa wanasema kuwa kimbunga hicho kitaikumba China upande wa pwani ya kusini mashariki leo Jumanne mchana.