BEIJING: Wachimba migodi 102 wamo hatarini
8 Agosti 2005Matangazo
Wachimba migodi 102 wamekwama katika mgodi wa makaa ya mawe uliofurika, kusini mwa China. Ajali hiyo imetokea katika mkoa wa Guangdong yapata mita 420 chini ya ardhi na waokoaji wanajaribu kuyavuta maji kutumia mitambo ili kuwaokoa wachimba migodi hao.
Migodi nchini China ndio migodi hatari kabisa duniani, huku wachimba migodi 2,700 wakiuwawa katika migodi hiyo kila miezi sita ya mwanzo kila mwaka.