Beijing. Virusi vya mafua ya kuku vyapatikana tena China.
6 Novemba 2005Zaidi ya kuku milioni moja wameamriwa kuchinjwa kaskazini mashariki ya China katika juhudi za kukabili kuzuka kwa ugonjwa wa mafua ya ndege. Shirika rasmi la habari la Xinhua limeripoti kuwa zaidi ya maafisa 1,700 wakisaidiwa na polisi wenye silaha , wamepelekwa katika jimbo hilo lililoathirika la Liaoning , kuwauwa kuku hao.
Hii inakuja siku mbili baada ya China kuripoti kuzuka kwa mara ya nne kwa virusi hivyo katika muda wa mwezi mmoja.
Karibu kuku 9,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa mafua ya ndege katika jimbo la Liaoning.
Virusi hivyo vimeuwa kuku milioni kadha pamoja na watu wapatao 60 katika bara la Asia katika muda wa miaka miwili iliyopita.