BEIJING: Raia warejea baada ya mlipuko wa gesi
30 Desemba 2003Matangazo
Raia wa China waliokuwa wamehamishwa makwao baada ya mlipuko wa gesi kutokea wiki iliopita kusini magharibi mwa nchi hiyo wameanza kurudishwa makwao. Vyombo rasmi vya habari mjini Beijing vimearifu kuwa maiti 35 zaidi zimepatikana na kufanya idadi jumla ya waliokufa kutokana na mlipuko huo kufikia sasa 234. Wataalamu wa mambo ya gesi na maafisa wa serikali ya China wanasema kuwa wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kutafuta kiini halisi cha ajali hiyo. Maafisa wa eneo hilo wanakana hata hivyo kuwa lilifanyika kosa la binadamu kusababisha msiba huo uliotokana na kuvuja kwa gesi kiwandani.