BEIJING: Ngawa 10,000 kuuwawa China kutokana na SARS
5 Januari 2004Matangazo
China imeamuru kuuwawa kwa ngawa takriban 10,000 katika jimbo lake la kusini la Guangdong baada ya utafiti kudokeza kwamba kuna uhusiano na kesi inayoshukiwa ya SARS ugonjwa wa homa ya mapafu. Watafiti katika Chuo Kikuu cha Hon Kong wanasema wamegunduwa mshabaha kati ya kijirusi kilichokutikana kwenye wanyama hao wa ngawa na mgonjwa anayeshukiwa wa SARS huko Guangdong na kudokeza kwamba ugonjwa huo asili yake yumkini ikawa inatokana na wanyama hao.Ngawa ambao sio jamii ya paka hupatikana katika mikahawa ya vyakula vya wanyama pori huko Guangdong.