BEIJING: Moto wa gesi wauwa mamia
25 Desemba 2003Matangazo
Watu zaidi ya 190 wamekufa katika mji wa kusini magharibi ya China wa Chongqing kutokana na ajali ya mlipuko wa gesi. Mlipuko umetajwa kuwa ulitokea jumanne usiku katika mgodi wa gesi wa Chuandongbei baada ya moja ya matanuri kupasuka na kuvujisha sehemu kubwa ya gesi na hewa ya hydroden. Imearifiwa kuwa zaidi ya watu elfu 95 na nusu wamekufa mwaka huu nchini China kutokana na ajali zinazohusiana na kazi viwandani.