BEIJING : Mkutano wa kihistoria kati ya China na Taiwan
30 Aprili 2005Matangazo
Rais Hu Juntao wa China na kiongozi wa upinzani wa utaifa wa Taiwan Lien Chan wamekubaliana kushirikiana kukomesha zaidi ya miaka 50 ya uhasama.
China inaiona Taiwana kuwa ni jimbo lililoasi na serikali ya Beijing inasema itachukuwa hatua ya kijeshi iwapo kisiwa hichi kitajaribu kujitangazia huru.Tafauti na uongozi wa hivi sasa wa Taiwan Lein anapendelea kuungana na Jamhuri ya China..
Serikali ya Taiwan inayopendelea uhuru imesema imekatishwa tamaa sana na ziara ya Lien nchini China na kusema kwamba jeshi la China bado linaendelewa kuwa tishio kwa wananchi wa Taiwan.