BEIJING : Mazungumzo ya nuklea yaahirishwa kwa wiki tatu
7 Agosti 2005Mazungumzo ya nchi sita kuishawishi Korea Kaskazini kutelekeza mipango yake ya kutengeneza silaha za nuklea yameahirishwa kwa wiki tatu baada ya wajumbe wake kushindwa kufikia muafaka.
Mjumbe mkuu wa China kwenye mazungumzo hayo Wu Dawei amewaambia waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa kikao cha awali leo hii kwamba mazungumzo hayo yataanza tena katika wiki ya mwisho ya mwezi wa Augusti.Muda huo unatowa nafasi kwa wajumbe kuripoti kwa serikali zao na kutatuwa hitilafu zinazoendelea kuwepo.
Mazungumzo hayo yanayozihusisha nchi mbili za Korea ile ya Kaskazini na Kusini,China,Japani,Russia na Marekani yameshindwa kutowa waraka wa pamoja unaoelezea vipi Korea ya Kaskazini itaachana na mipango yake ya silaha za nuklea na kile itakachopatiwa badala yake.