BEIJING: Matumainio ya kuwaokoa wachimba-migodi yafifia
9 Agosti 2005Matangazo
Kuna khofu kuwa hadi wafanyakazi 116 wamepoteza maisha yao katika ajali 2 mbali mbali zilizotokea katika migodi kusini mwa Uchina.Kwa mujibu wa vyombo rasmi vya habari,hakuna matumainio ya kuwaokoa wachimba-migodi 102 walionasa katika mgodi uliojaa maji.Maafisa wamesema,ukiukaji wa utaratibu wa usalama umesababisha ajali na wamewataka mameneja 65 waliotoroka,warejee kwenye eneo la ajali.